Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Mhina Donati amewataka Wazee kutumia busara walizonazo kuongea na Vijana wao, ili washirikiane kwa pamoja kulinda Maadili ya watoto katika kijiji chao.

ASP Mhina ameyasema hayo katika kijiwe cha mchezo wa draft cha wazee hao kilichopo kijiji cha Sanganjeru kata ya Madege iliyopo Wilayani Gairo Mkoani Morogoro.

Mara baada ya kuongea na Wazee hao ASP Mhina alielekea Shule ya Sekondari Madege kwa lengo la kutoa elimu kwa Wanafunzi wa Shule hiyo, ambapo aliwafundisha mambo mbalimbali kuhusu kujilinda na kuepuka vitendo hatarishi.

Ameyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na kujilinda dhidi ya unyanyasaji na ukatili huku akiwapa njia za kutoa taarifa, elimu kuhusu Mradi wa ‘Ongea Nao’ na kuwasisitiza kwenda kuwasaidia wazazi wao kazi za nyumbani baada ya kumaliza mitihani yao.

Real Madrid yakanusha mpango wa Mbappe
Parimatch, Tigo Pesa wazindua promosheni Vibunda Spesho