Koplo wa Polisi, David Donni wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na wizi wa Mifugo (STPU), amewataka Wananchi jamii ya wafugaji kuacha kuwatumia watoto kwenye kuchunga mifugo badala yake wawapeleke shule, kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria.

Koplo David ameyasema hayo wakati akitoa elimu kwa wafugaji hao katika Mnada wa kuuza Mifugo uliopo Kijiji na Kata ya Mziha Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Aidha, aliwataka Wafugaji hao kuvusha mifugo yao kwenye sehemu zilizotengwa kwa ajili ya kuvusha ili kuepuka ajali kwenye barabara kuu.

Hata hivyo, amewataka Wafugaji hao kujenga Mazizi imara, ili kuzuia wezi kuiba kirahisi kushiriki kwenye vikundi vya Ulinzi Shirikishi na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Carlo Ancelotti: Nina washambuliaji wa kutosha
Kocha Namungo FC atamba kuibanjua Simba