Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Hospitali ya Queen Elizabeth ya nchini Uingereza, inatarajia kuweka kambi maalumu ya upasuaji wa kuweka nyonga na magoti bandia kwa wagonjwa wenye changamoto za maradhi hayo kuanzia Oktoba 27, 2023 – Novemba Mosi 2023.

Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Upasuaji Mifupa, Nyonga na Magoti, Dkt. Shilekirwa Makira amesema wagonjwa watakaonufaika na huduma hizo ni pamoja na wenye matatizo ya nyonga zilizosagika zenye maumivu makali na magoti yaliyosagika.

Amesema, “watu wajitokeze na kujisajili mapema kabla ya tarehe 27 /11/ 2023 ili Hospitali iweze kufanya maandalizi stahiki ikiwemo pamoja na kufanya vipimo vya awali ambayo ni muhimu kabla ya kufanya upasuaji huu.”

Aidha, Dkt. Makira ameongeza kuwa wale waliojiunga na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya, mfuko unagharimia zaidi ya asilimia 90, pia Bima zingine zinagharimia matibabu haya hivyo wasisite kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo adhimu.

Kapinga awataka wasimamizi Miradi ya REA kuongeza ufanisi
Waliofariki kwa mafuriko Kenya wafikia 15