Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini – DCEA, imewakamata watu 16 wanaojihusisha na shughuli za utengenezaji wa Biskuti kwa kuchanganya na bangi aina ya skanka, huko Kawe Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, Aretas James Lyimo amesema watuhumiwa hao wamekutwa wakiendelea na uzalishaji wa Biskuti hizo kwa kutumia mtambo mdogo wa kusaga skanka na vifaa vya kutengenezea biskuti hizo za bangi.

Amesema, kutokana na operersheni hiyo watu hao wamekamatwa na Kilogramu 423.54 za bangi iliyosindikwa ya skanka yenye kiwango kikubwa cha sumu ya TetraHydro Cannabinol THC.

Kiwango hicho ni kikubwa, ikilinganishwa na asilimia 3 hadi 10 zilizo katika bangi ya kawaida huku neno Skanka likiwa ni jina la mitaani linaloitambulisha Bangi hiyo yenye kiwango kikubwa cha Sumu.

Nicolas Jackson afurahia Hat-Trick
Watumishi wa Serikali kizimbani matumizi mabaya ya madaraka