Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Mkoani Pwani, Mwinyishehe Mlao amewataka Wajumbe wa Halmashauri kuu ya chama hicho Mkoa kuzingatia katiba ya chama kwa kutumia busara kuwaonya na kuwarekebisha Viongozi wa Serikali.

Mlao ameyasema hayo mjini Kibaha wakati akifunga Kikao cha kawaida cha Halmashauri kuu ya CCM Pwani na kuongeza kuwa Viongozi wa chama na Serikali wote ni wamoja na wanastahili heshima.

Amesema,”inawezekana Viongozi wa serikali wakawa wamekosea lakini ni lazima kuangalia kiongozi huyo wa serikali anajadiliwa wapi na unazungumza nae wapi maana kila mtu anastahili heshima ya kuthaminiwa utu wake.”

“Kila mtu hapendi kuumbuliwa hata kama kiongozi huyo anaweza kukuambia jambo na wewe ukaelewa kabisa kwamba kiongozi huyo anakuongopea kuwa na hekima tulia baadae kwa busara ndipo umweleze ukweli unaoufahamu hapo hamtagombana,” amesema Mlao.

Malisa ataka usajili wa Vyuo uhakikiwe Mbeya
Rais samia avunja Bodi TCRA, afanya teuzi