Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, imesema itaendelea kuwasilisha taarifa kuhusu utatuzi wa changamoto za Muungano unaofanyika kupitia vikao baina ya Serikali zote mbili.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Asya Mwadini Mohammed aliyetaka kujua kama Serikali haioni haja ya kuwasilisha Bungeni taarifa za mchakato wa utatuzi wa changamoto za Muungano.

Amesema, hivi karibuni katika vikao vya Kamati za Bunge, miongoni mwa taarifa zilizowasilishwa ni pamoja na ile inayozungumzia Changamoto za Muungano zilizotatuliwa na zile ambazo zinaendelea kutatualiwa ili wananchi wapate ufahamu wa kazi hiyo kubwa inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo.

“Nimpongeze mbunge kwa swali lake zuri na tunaahidi kuwa tutaendelea kuleta taarifa za kila tunapotatua changamoto hizi za Muungano katika Bunge lako tukufu Naibu Spika hususan katika kipindi cha bajeti na tutaendelea kufanya hivyo kwa vikao vijavyo,“ amesisitiza Dkt. Jafo.

Awali, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis akijibu swali la Mbunge wa Konde Mhe. Mohamed issa, amesema tangu kuasisiwa kwa Muungano Serikali zliona haja ya kuunda kamati ya kutatua changamoto katika ngazi mbalimbali.

Maagizo ya lazima yaliniondoa CCM - Bwege
Almanusura ya wachezaji Simba SC