Klabu ya Tottenham Hotspur imepata pigo zaidi baada ya kuthibitisha kwamba Mshambuliaji wake, Richarlison atalazimika kufanyiwa upasuaji wa nyonga jambo litakalomweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Brazili amekiri kusumbuliwa na maumivu makali kwa miezi ya hivi karibuni.

Mashabiki wa Spurs wanafahamu wazi mchezaji wao mwingine Micky van de Ven atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kupata maumivu ya misuli ya paja kwenye mechi ya kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Chelsea, Jumatatu (Novemba 06).

Kiungo James Maddison naye aliumia enka katika mechi hiyo, wakati kikosi hicho kitawakosa pia Ivan Perisic, Manor Solomon na Ryan Sessegnon kutokana na kuwa majeruhi. Na sasa Richarlison atafanyiwa upasuaji.

Mshambuliaji huyo wa Pauni 60 milioni, alisema: “Miezi ya karibuni imekuwa migumu sana kwangu. Nimekuwa kwenye matatizo makubwa ya kiafya. Nimeshazungumza na madaktari na kinachotakiwa ni upasuaji wa nyonga.”

Van de Ven na Maddison walitarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi juzi Jumanne ili kuona ukubwa wa tatizo baada va kuumia kwenye mchezo wa Chelsea.

Spurs itawakosa pia Destiny Udogie na Cristian Romero dhidi ya Wolves baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu ilipocheza na Chelsea Jumatatu (Novemba 06).

Mila: Wafanya tamasha kumuaga marehemu
Maagizo ya lazima yaliniondoa CCM - Bwege