Kama tunavyoendelea kujifunza na kufahamu kwamba Duniani kuna Makabila mengi ambayo yana utamaduni wake, lakini baadhi ya tamaduni za makabila hayo tumeona kwamba zimekuwa zikishangaza na kuacha maswali, kutokana na utaratibu husika wa maisha yao.

Huko Malawi, kuna Kabila linalofahamika kama Wachewa, wao ni Wabantu lakini kama ilivyo kwa makabila mengine ambayo hayakosi utaratibu wao wa maisha unaoshangaza, basi hawa ndugu zetu nao wana kanuni zao zenye vipengele matata sana.

Ipo hivi, Mtu akifa wao huandaa Tamasha la mazishi, halafu wakati wa sherehe hiyo ya mazishi ya mshiriki wa kabila lao, ni kawaida kwa mwili wa marehemu kuoshwa ambapo mwili wa marehemu hupelekwa mahali wao wanapopaita ni patakatifu na kufanya utakaso kwa kumkatwa koo marehemu na kisha kumwagia maji ili yaingie ndani ya maiti.

Kinachofuata ni kukaa kwa muda fulani kisha kuanza kuukamua mwili huo maji hadi yatoke safi. Kisha maji hayo huhifadhiwa ili yatumike kuandaa chakula cha jamii nzima iliyoshiriki tukio la mazishi wakiamini kwamba kifo huletwa na Wachawi na hutumia njia hiyo kuona ni nani hataweza kula ili kukamata uchawi ni lazima mtu akifa Kijiji chote kihudhurie.

Hoja kuu hapa ni kwamba ambao wanaweza kumuua mtu wangeogopa kwenda kwenye mazishi na ifahamike kwamba Wachewa wenye wakazi wapatao milioni 1.5 wana koo mbili za Waphiri na Wabanda, lakini Waphiri wanahusishwa na wafalme na aristocracy, wakati Banda kwa kawaida ni waganga na mafumbo.

Utamaduni, Sanaa havitenganishwi - Dkt. Muyonga
Spurs kumkosa Richarlison kwa miezi kadhaa