Lydia Mollel – Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilombero ili kukamilisha mradi wa Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Lipangalala iliyopo Wilayani humo, kutokana na kusua kwa ujenzi wake hadi sasa ambao hauridhishi.

Malima amesema, kuchelewa kwa mradi huo kumetokana na mgogoro wa mda mrefu kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Lena Mkaya na Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Abubakary Asenga, unaokwamisha jitihada za Serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Aidha, Malima pia ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, kufanya uchunguzi wa kina kuhusu kile kinachosababisha kukwama kwa mradi huo na kutumia fedha nyingi zaidi ya milioni 528.

Mradi huo, ulipangwa kukamilika Oktoba 2023, lakini hadi sasa haujakamilika kutokana na mgogoro huo na Mkuu huyo wa Mkoa amesema mradi huo unatakiwa ukabidhiwe Januari Mosi 2024, ili Wanafunzi waweze kuanza masomo.

Simba SC: Tunaimani na Matola, Cadena
Madiwani Chalinze wapitisha wazo la Nyota tano