Mwanasiasa mashuhuli na aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Seleman Bungala ‘Bwege’ ameitaka Serikali kutekeleza sera zake kwa vitendo na kufanyia kazi maoni ya Wananchi na yale yanayotolewa na Vyama vya upinzani na endapo itashindwa kufanya hivyo, iondoke madarakani.

Bungala ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalum na Dar24 Media Nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa wao kama Wanasiasa, ni wajibu wao kuikosoa Serikali kwa yale ambayo wanaona yana ulazima katika kufanyiwa kazi kwa maslahi ya Taifa na si kupuuzwa.

Amesema, “na katika hili aidha watekeleze nchi iende au wasitekeleze watoke nadarakani, kwasababu sisi Wanasiasa tuna mambo mawili tu, tunataka dola na tunataka maisha mazuri, kama CCM inafanya mambo mazuri watu wanapata manufaa, watu wanapata haki, uhuru upo, maendeleo yanapatikana sasa hapo unakuwa mpinzani wa nini sasa?.”

Hata hivyo, Bwege amesema ili kuwa mpinzani wa kweli ni lazima uwe katika misingi ya kudai haki, uhuru na Demokrasia na kwamba uhitaji wao wa kutaka kushika dola hutokana na Serikali iliyopo madarakani kwenda kinyume na mambo hayo na hivyo kuona haifai kuongoza nchi.

Tushirikiane kutokomeza tatizo Watoto Njiti - Serikali
Majaliwa ataka ufanisi mipango maendeleo ya Taifa