Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko amewataka wadau wa masuala ya Afya ya Watoto nchini, kushirikiana kutokomeza tatizo la watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto Njiti).

Wito huo, umetolewa wakati wa hafla ya kusherehekea mafanikio ya Ajenda ya Mtoto Njiti (2021) iliyofanyika jijini Dodoma na kuongeza kuwa, takribani watoto milioni 15 duniani huzaliwa Njiti huku nchi za Bara la Asia na Afrika hasa kusini mwa jangwa la Sahara, zikiongoza kwa asilimia 80 ya vifo vya watoto hao.

Amesema, “inakadiriwa kila mwaka watoto 336,000 huzaliwa njiti nchini Tanzania na zaidi ya watoto 11,500 hupoteza maisha kutokana na changamoto za kuzaliwa njiti. Ni kweli kwamba kiwango cha kuzaliwa kwa watoto njiti hapa nchini kimekuwa kikiongezeka. Hatuna budi kuzidisha mapambano na ningefurahi siku moja itokee taarifa kuwa hakuna vifo vya watoto njiti nchini kwetu.”

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ridhwan Kikwete amesema akipata nafasi ya kuwasilisha hoja kuhusu sheria ya utumishi na likizo ya uzazi atashauri likizo ya uzazi ifikie miezi sita, ili watoto njiti wapate malezi stahiki.

Mchakato kurejesha kumbukumbu za Tanzania waanza
Tekelezeni sera Nchi iende au tokeni madarakani - Bwege