Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imeweka kipaumbele kikubwa katika sekta ya elimu kwa kuongeza bajeti, kuimarisha miundombinu kwa kujengwa shule zenye vifaa vya kisasa, pamoja na kuajiri walimu wa masomo ya sayansi ili kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo katika hafla fupi ya chakula cha mchana na kuwapongeza wanafunzi waliopata ufaulu wa daraja la kwanza kwa kidato cha nne mwaka 2022 na kidato cha sita mwaka huu aliyowaandalia viwanja vya Ikulu Zanzibar hii leo Novemba 12, 2023.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itahakikisha inaongeza fedha ili kila mwanafunzi mwenye nafasi ya kuendelea na masomo ngazi ya elimu ya juu anapatiwa mkopo.

Vilevile Rais Dkt. Mwinyi ametoa zawadi ya laptop moja kwa kila mwanafunzi aliyefaulu kiwango cha daraja la kwanza wa kidato na nne na sita kwa skuli za Unguja na Pemba jumla 1,450.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 13, 2023
Makonda ataka kasi ujenzi daraja la Kigogo - Busisi