Kamati ya Siasa, ikiongozwa na Katibu Wa Itikadi na uenezi – NEC, Mkoa wa Dodoma Jawadu Mohammed imewapongeza Wasimamizi wa Miradi inayotekelezwa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, ikiwemo Shule na Hospitali kwa kuzingatia ubora na ufanisi unaotakiwa.

Akizungumza na baadhi ya Viongozi walioshiriki katika ziara ya ukaguzi wa Miradi hiyo, Jawadu amewataka watumishi wa Umma kuitangaza na kuwa Mabalozi Wazuri wa Miradi inayotekelezwa na Serikali huku akisisitiza suala la upandaji Miti kwa Kila mradi, ili kuhakikisha mazingira yanakuwa bora na imara hivyo kudumisha Sera ya Serikali ya Mkoa ya “Kijanisha Dodoma”.

Amesema, “ni lazima tuwe na watu makini wa kufuatilia miradi inayoletwa na Rais wetu ili wananchi wasiwe na changamoto katika kupata huduma na ndio maana zimejengwa shule na Hospitali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na zinazostahili.

“Serikali ipo imara na imedhamiria kuhakikisha wananchi wanapata huduma za umeme, maji, mabweni, madarasa na majengo yote yanakua kwenye ubora na uimara wa Hali ya juu.Ni lazima miundombinu zote zikamilike kwa wakati kama mikataba inavyotaka hatufikirii kuona miradi inavuka muda wake wa utekelezaji,” Amesema Mohamed.

Kamati hiyo, pia ilipata fursa ya kutembelea mradi wa Barabara kwa kiwango cha lami uliogharimu Kiasi cha Shilingi Milioni 599, ujenzi wa kituo cha afya Farkwa uliopokea kiasi cha Shilingi Milioni 500, Ujenzi wa Shule ya Msingi na awali Sankwaleto uliopokea kiasi cha shilingi Milioni 396, ujenzi wa Zahanati ya Sankwaleto wa Shilingi 97 Milioni na ujenzi wa Mradi wa maji Babayu Sshilingi 434 Milioni.

Ukaguzi wa Miradi mbalimbali unaofanywa na Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wa Kamati Mohhamed, ni muendelezo wa ziara ya kikazi wanayoifanya katika halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Dodoma.

Rais Samia amedhamiria kuwaletea maendeleo - Dkt. Biteko
Victor Osimhen afunguka alivyoitosa Al Hilal