Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi – DECOHAS, kimejipanga kurudisha kozi ya Afya ya Afua ya Jamii ambayo hivi karibuni ilifutwa kutokana na sababu mbalimbali na kuleta mjadala katika mitandandao mbalimbali ya kijami.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika kuelezea maadhimisho ya miaka 10 ya chuo na mahafali ya saba hii leo Novemba 15, 2023 Jijini Dodoma, Makamu Mkuu wa Taaluma, utafiti na Uelekezi – DECOHAS, George Adriano amesema, wapo katika Mchakato wa kurudisha kozi hiyo.
Amesema, DECOHAS inajivunia kuwa na Wanachuo zaidi ya 3,000 katika kampasi zote mbili na Wanachuo 4944 ambao wamemaliza wapo katika soko la ajira na wameajiriwa Serikalini na kwamba Desemba 15 2023 kutakuwa na sherehe ya maadhimisho ya miaka 10 ya DECOHAS itakayoambatana na mahafali ya saba yatakayofanyika kampasi ya Nala.
“Zaidi ya Wanachuo mia saba (700) wanatarajia kuhitimu masomo yao siku hiyo na mgeni rasmi atakuwa kiongozi mkubwa ambapo atatangazwa hivi karibuni akiambatana na msanii mkubwa Tanzania Rayvany kwajili ya kutoa burudani,” amesema Adriano.