Gary Neville anaamini kwamba, Arsenal wanaweza kushinda Ligi ya Premier msimu huu, lakini bado ana wasiwasi na ubora wa safu ya ushambuliaji waliyo nayo.
Arsenal wameanza vyema msimu huu licha ya kushindwa kufikia kiwango chao cha msimu uliopita ambao walipambana hadi mwisho, wakakaribia kuwa mabingwa, wakaishia nafasi ya pili.
Hivi sasa Arsenal chini ya Mikel Arteta, ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Premier nyuma ya vinara Manchester City waliokusanya pointi 28, wakifuatiwa na Liverpool (27) ambao wana pointi sawa na Arsenal baada ya zote kucheza mechi 12.
“Nafikiri Arsenal wanaweza kushinda ligi msimu huu. Licha ya kuanza polepole, lakini watakuja kukaa sawa mbele na kufanya vizuri kama tulivyoona msimu uliopita.
“Ukweli ni kwamba wameanza polepole kidogo, sidhani kama ni jambo baya. Wasiwasi wangu kwa Arsenal ni Mshambuliaji wa kati, nawapenda (Gabriel) Jesus na (Eddie) Nketiah, lakini kwangu mimi ni namba mbili na tatu, wanahitaji mshambuliaji namba moja,” alisema Neville.