Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amefanya ziara maalumu ya Kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya miundombinu ya Barabara katika Wilaya ya Kiteto na kutoa agizo la kufanya kazi usiku na mchana ili Wananchi waweze kuendelea na shughuli za kimaendeleo.

Katika ziara hiyo, RC Sendiga amekagua miradi ya Barabara ya Ngipa- Ndirigishi na Engusero-Kiperesa, ambayo inafanyiwa ukarabati na maboresho, ikijengwa kwa kiasi cha shilingi 681.5 Milioni ambao utawanufaisha wakazi wa maeneo hayo na jirani.

Aidha, ametoa maelekezo kwa TARURA kukamilisha miradi hiyo kwa muda ambao umepangwa na ameagiza kazi zifanyike usiku na mchana, ili wananchi waweze kupata huduma zao kama hapo awali bila kuathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Hata hivyo, Sendiga pia amesisitiza suala la upandaji Miti pembezoni mwa kingo za madaraja, ili kulinda mmomonyoko wa udongo pembezoni mwa madaraja yanayojengwa na yaliyokwisha kukamilika.

Abdelhak Benchikha anukia Simba SC
Simba SC waivalia njuga ASEC Mimosas