Kikosi cha Al Hilal ya Sudan inayonolewa na kocha maarufu Afrika, Florent Ibenge kipo nchini Tanzania na leo Ahamis (Novemba 16) jioni kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya KMC kwenye Uwanja wa Baobab kuanzia saa 8:00 mchana.

Mchezo huo utakuwa wa ndani ukiwa unalenga kujifunza na kubadilishana ujuzi kwa pande zote mbili huku pia wakifanya mazoezi ya pamoja ikiwa ni maandalizi ya mechi ijayo ya Ligi dhidi ya Kagera Sugar kwa KMC, huku kwa Hilal ikiwa ni maandalizi ya mechi ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro de Luanda, Novemba 25.

Kocha mkuu wa KMC, Abdihamid Moallin alisema; “Ligi kwa sasa imesimama, tumeendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi zijazo. Tulihitaji mechi za kirafiki na kwa bahati nzuri tumeipata Hilal moja ya timu bora Afrika na tutashirikiana nao.

“Pamoja na yote tutacheza mechi ya kirafiki itakayotupa tathimini ya kikosi chetu kabla ya kuendelea na ligi tutakapowakabili Kagera”

KMC ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi tisa ikivuna pointi 15, na mchezo ujao itacheza ugenini Kaitaba Bukoba, dhidi ya Kagera Sugar iliyo nafasi ya nane na alama 12. Mechi itapigwa Novemba 22, 2023.

Polisi kuwasaka Mgambo waliomjeruhi Mama kwa kipigo
Abdelhak Benchikha anukia Simba SC