Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema Uongozi wa Klabu hiyo umeyaona Mabango ya barabarani yaliyowekwa na Watani zao wa jadi Young Africans.

Young Africans imesambaza mabango hayo katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam tangu Jumanne (Novemba 14), ikiwa ni sehemu ya shamra shamra ya ushindi wa mabao 5-1 walioupata dhidi ya Simba SC, Novemba 05.

Ahmed Ally amekiri kuonwa kwa mabango hayo alipozungumza na waandishi wa habari leo Ahamis (Novemba 16), ambapo amesema wamekuwa wakipokea ushauri mbalimbali wa kisheria na kama itaonekana inafaa kuchukua hatua au kuacha watafanya hivyo.

“Kuhusu mabango tumeyaona na tuna kitengo cha sheria, wanaangalia kuona kama inafaa kuchukua hatua au kuacha lakini hili tumesababisha sisi. Wakati ujao wachezaji wafanye kila linalowezekana hiyo kadhia isitokee tena. Mwiba unatokea ulipoingilia.”

Wachezaji Simba SC waombwa kupambana

“Yaani kama kuna mchezaji ameyaona hayo mabango anapaswa kufahamu kwamba, yeye ndio kasababisha hayo yote, kwa hiyo itamlazimu kupamabana ili kutuondolewa kadhia hiyo.” Amesema Ahmed Ally

Southgate amchefua Rio Ferdinand
Ahmed Ally: Tuzo ya AFL haitakaa ofisini