Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia doria ya pamoja, wamefanikiwa kukamata watuhumiwa wawili wakiwa na jumla ya mifugo 303 ambayo walikua wanaisafirisha kwenda Nje ya Nchi kwa njia za magendo bila kuwa na vibali.

Akiongea katika Mnada wa Longido, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Simon Pasua leo Novemba 19, 2023 amebainisha kuwa mifugo hiyo pamoja na watuhumiwa hao wamekamatwa maeneo ya Buguruni C, Wilaya ya Longido Mkoani Arusha.

Amesema, bado wanaendelea na upelelezi, na pindi utakapokamilika watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria huku akitoa wito kwa wafugaji kuacha tabia ya kutorosha mifugo kwenda Nje ya Nchi bila ya kufuata utaratibu wa kupata vibali toka Serikalini.

Kwa upande wake Daktari wa Mnada wa Longido, Ally Hamka amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni baadhi ya wafanyabaishara wa mifugo kutokuwa waaminifu kwa kukwepa kupeleka mifugo yao katika mnada huo kwa ajili ya kupewa vibali.

Naye Joseph Lengashe ambaye ni mfugaji na mfanyabiashara amewaasa wafanyabishara wenzake kufuata utaratibu uliwekwa na Serikali wa kupata vibali vya kusafirisha mifugo yao kihalali, ili kuepuka hasara ambazo wanaweza kukutana nazo pindi itakapokamatwa na kutaifishwa.

Liberia: Wananchi waonesha nguvu ya mpiga kura
CCM wahimiza kusomesha Watoto manufaa fursa za uwekezaji - Mlao