Leo, Novemba 20, 2023 Taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linaanza kampeni za uchaguzi wa rais kwa mwezi mmoja kwa kuhusisha wagombea 26 wanaowania urais, huku kukiwa na hali ya wasiwasi wa kisiasa na mapigano yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Takriban wapiga kura milioni 44 waliojiandikisha, kati ya wakazi karibu milioni 100, watashiriki zoezi la kumchagua Rais wa Taifa hilo Desemba 20, 2023.

Waoigq kura hao pia watawachagua wagombea ubunge na wajumbe wa Serikali za Mitaa katika nchi hiyo yenye rasilimali nyingi, lakini imegubikwa na migogoro na ufisadi.

Hata hivyo, Rais wa DRC Felix Tshisekedi anadaiwa kuanza kampeni za mapema nje ya utaratibu akiwania muhula wa pili wa kuliongoza Taifa hilo akihudhuria hafla nyingi za umma na washirika wake kusifia rekodi yake za uongozi.

Wahitimu wapewa mbinu kuepuka matukio ya uhalifu
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 20, 2023