Beki wa Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Kim Min-Jae ameibiwa nje ya nyumba yake wakati anahamia kwenye makazi mapya kwa mujibu wa ripoti.

Beki huyo kutoka Korea Kusini alikamilisha usajili wa kujiunga na miamba hiyo ya Munich, akitokea kwa mabingwa wa Soka nchini Italia SSC Napoli wakati wa Dirisha la usajili mwanzoni mwa msimu huu, na akakumbana na janga hilo.

Beki huyo akiwa na mabingwa hao watetezi wa Bundesliga akiwa amecheza mechi 17 chini ya Thomas Tuchel, lakini akini kwa mujibu wa ripoti ilitolewa na jarida la Ujerumani la Bild, beki huyo alifanyiwa uovu wakati akihamia kwenye nyumba yake mpya.

Kim aliweka jiko la kupikia chakula kando ya nyumba yake ili kuingiza sanduku ndani lakini aliporudi jiko hilo halikuoneka, hapo ndipo akagundua ameibiwa.

Ripoti hiyo iliendelea kufichuliwa mshauri wa beki huyo, Kim Dee Hong alileta jiko jipya la kupikia wali kutoka Korea Kusini ili kufurahia chakula cha asili yao.

Jiko lilikuwa ndo kitu muhimu zaidi kwa beki kwa sababu chakula aina ya wali ni maarufu sana huko Korea hivyo alisikitika baada ya kuibiwa kwa mujibu wa ripoti.

Everton hatarini kulimwa Point nyingine
Serikali yawahakikishia Watanzania uhuru wa mawazo