Klabu ya Everton ipo katika hatari ya kupunguzia pointi kwa mara ya pili kwenye Ligi Kuu England kwa mujibu wa ripoti.

Tume huru itafanya maamuzi kama Toffees inastahili kupokonywa pointi zaidi huku klabu tatu Burnley, Leeds United na Leicester City zikipanga njama ya kudai fidia ya Pauni 300 milioni kutoka kwao.

Gazeti la Daily Mail linadai kwamba ikiwa timu hizo zitashinda madai yao, Everton itapunguzwa pointi nyingine na huenda ikawa katika hatari kwenye soko la kibiashara.

Everton inatarajiwa kununuliwa na kampuni ya 777Partners, lakini kampuni hiyo italipa pesa nusu iwapo itashushwa daraja au endapo italipa fidia kwa timu nyingine.

Everton ilipunguzwa pointi 10 wiki iliyopita kutokana na kukiuka kanuni za matumizi ya pesa Ligi Kuu England ambazo zilizidi kiwango.

Lakini Everton itakata rufaa dhidi ya uamuzi huo na gazeti la The Telegraph linasema watapambana vikali dhidi ya jaribio lolote la kuwalazimisha kulipa fidia kwa timu nyingine. Everton, ambayo haijafungwa katika mechi nne zilizopita, itakata rufaa dhidi ya adhabu hiyo iliyotolewa wiki iliyopita.

Simba SC yahamisha kambi kwa Radhi Jaidi
Kumbe Kim Min-Jae alipata majanga Munich