Ofisi za Taifa za Takwimu barani Afrika zimetakiwa kuendelea kuzalisha Takwimu rasmi, zenye ubora na kuzisambaza kwa njia rafiki na za kuaminika kwa wakati, ili kuwezesha Serikali na wadau kufanya maamuzi yanayohusu utekelezaji wa eneo huru la biashara.

Hayo yamesemwa hii leo Novemba 20 Jijini Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabiri Shekimweri wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika na amesema Ofisi hizo hazina budi kuboresha mifumo ya ushirikiano kitakwimu, ili ziweze kuwafikia wadau kwa urahisi.

Amesema, “kwa kushirikiana na Ofisi za Takwimu za Afrika zitakuwa zinatekeleza lengo namba 17 la malengo endelevu ya Dunia ambalo linahimiza ushirikiano katika kutekeleza malengo hayo ambayo Nchi za afrika zimeridhia utekelezaji wake.”

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu NBS, Emilian Karugendo amesema matumizi ya Takwimu rasmi ndio msingi wa kila kitu katika maisha,katika mipango na katika kufuatilia programu mbalimbali na utekelezaji wake.

Jezi ya Lionel Messi kuuzwa Mabilioni ya Shilingi
Saratani shingo ya kizazi: Ukiweza inawezekana