Wananchi walio wengi wamekuwa wakishindwa au kuhofia kufika ili kupata huduma katika ofisi za Umma, kutokana na uwepo wa malalamiko ya vitendo vya Rushwa ndogondogo kwa baadhi ya Watendaji Serikali wasio waaminifu.

Kauli hiyo imetolewa na WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene katika mkutano Mkuu wa mwaka wa  viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) unaoingia siku yake ya pili jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamisha wa Polisi, Salum Hamduni akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene tuzo ya kuthamini mchango wake katika mapambano dhidi ya rushwa jijini Dodoma.

Amesema, “bado suala la rushwa ndogondogo ni tatizo sana kwa Wananchi wetu na huko ndiko yapo malalamiko mengi ya watu kutokana na rushwa hiyo kuwanyima fursa ya kupata huduma, jambo hili linawakera Wananchi hivyo lazima kuwa na mikakati ya kuhakikisha zinazuiliwa.”

Sehemu ya washiriki wa  Mkutano Mkuu wa mwaka wa  viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) unaofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.

Aidha, Simbachawene amesema ipo haja ya kutengeneza sheria za kuwashughulikia viongozi walioshiriki katika masuala ya rushwa  wanapostaafu, ili kutoa funzo kwa Viongozi wengine.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Kamishna wa Polisi Salum Hamduni, akizungumza katika mkutano huo amesema katika mwaka wa fedha uliopita taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa Shilingi 171.9 Bilioni.

Kocha CR Belouizdad aipa heshima Young Africans
Mapigano ya kikabila yauwa 32