Serikali imeweka kwenye Sheria kiwango cha thamani ya miradi iliyokuwa ikitekelezwa na wazawa kutoka shilingi bilioni 10 hadi shilingi bilioni 50, ili kuwawezesha wazawa kunufaika na kuwafanya wawe walipakodi wakubwa kwa maendeleo ya nchi.

Kauli hiyo imetilewa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba wakati wa Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali, Makandarasi na Washauri Elekezi wa Ndani ulioangazia nafasi yao katika utekelezaji wa miradi.

Amesema, “Sheria ilikuwa inawapa local content Wakandarasi bora ambao ni wazawa lakini kwa sasa wazawa wanaruhusiwa kupata mradi wenye ukubwa wowote na kuruhusiwa kuajiri wakandarasi wengine kutoka nje kwa miradi wanayotekeleza.”

Kuhusu malipo ya Wakandarasi, Dkt. Nchemba alisema kila mwaka Serikali inatenga fedha za kulipa madeni na miradi inayoendelea ambapo inatenga zaidi ya shilingi bilioni 600 kwa ajili ya kuwalipa Wakandarasi, watoa huduma na wazabuni.

Serikali yawatoa hofu Wananchi, taarifa mgonjwa mpya wa Surua
Tuhuma: Walimu wadaiwa kula Chakula cha Wanafunzi