Serikali imekabidhi vifaa tiba Mkoani Singida vyenye
thamini takribani shilingi 472 Milioni, vitakavyotumika kuhudumia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kwenye Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, Kituo cha Afya Sepuka na Hospitali ya Wilaya ya Singida, Ilongero huku Mbunge wa Singida Mashariki akisema jamii ikiwa na afya njema itawajibika.

Vifaa hivyo, vimetolewa katika hafla iliyoshuhudiwa na Wabunge, Watendaji wa Idara mbalimbali za sekta ya Afya na Wananchi, ambapo Meneja wa Bohari Kuu ya Madawa – MSD Kanda ya Dodoma, Mwanashehe Jumaa amesema kazi ya usambazaji wa vifaa ni jukumu walilopewa na Serikali.

Amesema, “Lengo kubwa la kupelekwa vifaa hivyo ni kuhakikisha huduma za uzazi zinaboreshwa, MSD katika wilaya hii imekamilisha vifaa ambavyo ilikuwa
imepokea fedha zaidi ya shilingi Millioni 300 ili kukamilisha usambazaji wake.”

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ameishukuru Serikali na MSD kwa kupeleka vifaa hivyo na kuelekeza kuwa Sekta ya Afya ni uhai na watu
wakiwa na Afya njema wataweza kuwajibika na kuendesha majukumu yao vizuri.

MSD yaimarisha mifumo usambazaji Dawa, vifaa Tiba

Mtibabu bora ya Kinywa, Meno kutiliwa mkazo
Urahisi wa huduma: Wenye Ulemavu waungwe mkono