Rais wa Kenya, William Ruto ametangaza vifo vya watu 70 waliofariki kutokana na Mvua za El Nino nchini humo huku akisisitiza kuwa Serikali itawajibika kwa uharibifu uliotokea na kuita mkutano wa baraza la Mawaziri kwa dharula.

Rais Ruto ametoa tangazo hilo hii leo Novemba 25, 2023 na kuliamuru Jeshi la Ulinzi la Kenya – KDF kutumia Helikopta kusambaza misaada katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko ili kuwasaidia Wananchi kuondokana na changamoto zinazowakabili hasa Dawa na Chakula.

Amesema, Wizara ya Barabara kwa ushirikiano na KeNHA, pia wanatakiwa kurekebisha barabara kuu zilizoharibika, ili shughuli za kiuchumi na huduma za  usafiri ziweze kurejea.

Kufuatia hatua hiyo, Ruto amesema kamati za maafa kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali, zitakutana Novemba 27, 2023 kujadili hatua mbalimbali za kuchukua na kukabiliana na adha kama hizo.

Wasiowajibika kwa Wananchi wakataliwa CCM
Waliopunguzwa kazini SGR wandamana kudai stahiki