Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Katibu wa NEC. Organaizesheni Taifa, Issa Haji Ussi Gavu amesema Chama cha Mapinduzi – CCM, hakiwahitaji Viongozi wa Mitaa, Vitongoji na Vijiji wasiowajibika kwa Wananchi.

Ussi ameyasema hayo wakati akihutubia Wazee wa CCM na Jumuia ya Wazazi wa Mkoa wa Pwani, kwenye mkutano uliofanyikq Kibaha mkoani Pwani wa kuzungumza na Wazee.

Amesema, “tumepata taarifa kuwa wapo baadhi ya Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa ambao wanashindwa kukidhi matakwa ya Katiba na kanuni yaani Viongozi wasiowajibika kwa Wananchi hivyo katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji mwakani wasipewe nafasi.”

“Kama Mwenyekiti wetu anashindwa kusitisha vikao wala mikutano ya kuelezea mapato na matumizi ya fedha Mwenyekiti huyo achaneni nae, tafuteni Mwenyekiti wa kijiji, mtaa au kitongoji atakayesimama mbele ya watu anaowaongoza ambaye wao wenyewe watakiri na kusema huyu ni kiongozi kweli,” alisisitiza Ussi.

Aidha amewataka wa viongozi wa CCM na wanaCCM kufanya vikao vya kikatiba ilikujua kero na changamoto zinazowakabili Wananchi wanaowaongoza na kuzitafutia ufumbuzi, kwani tatizo kubwa la Viongozi ni kutotimiza vikao vya kikatiba na vya kikanuni vya ndani ya CCM.

Amesema kwa mujibu wa ibada 124 ya Katiba ya CCM Wazee ni taasisi na wanatakiwa kuhudhuria vikao harali vya ndani ya CCM na kuongeza kuwa, “rudini mkasome kanuni toleo la mwaka 2019 kuanzia ibada ya tatu ambayo inaelezea madhumuni na muhimu wa Baraza la Wazee kwa ngazi ya msingi imeanzishwa Baraza hili la Wazee kwa lengo la kurithisha tabia Njema kwa taifa letu.”

Naye Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge akifafanua changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na Wazee hao amewaomba watoe ushirikiano wa kuzingatia sheria na kanuni za Nchi katika kumaliza migogoro ya Wakulima na wafugaji mkoa wa Pwani ikiwa ni pamoja na kuunga mkono kuanzishwa kwa Ranchi ndogo za mifugo mkoani humo.

Amewata Wazee hao kuzingatia malezi Bora kwa watoto wao, ili kuepusha Mkoa huo na Taifa kwa ujumla kuondokana na kizazi kisicho na matendo yasiyo ya kimaadili, yanayowaingiza kwenye makundi ya uhalifu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Mafia, Hamisi Mbangu ameomba kuhimarishwa kwa usafiri wa anga na usafiri wa kwenye maji kwenda na kurudi katika kisiwa cha Mafia.

Prof. Mbarawa amtaka Mkandarasi kuongeza kasi
Kenya: 70 wafariki kwa El-nino, Rais aitisha mkutano wa dharula