Vijana Nchini, wametakiwa kutambua kwamba wana mchango mkubwa kwenye jamii katika juhudi za kuzuia na kupambana na vitendo vya uhalifu na wahalifu sambamba na matumizi ya Dawa za kulevya.

Kauli hiyo, imetolewa na Mkaguzi wa shehia ya Mtopepo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Masoud wakati akitoa elimu katika maskani/vijiwe mbalimbali katika shehia hiyo iliyopo Wilaya ya Magharibi A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Amesema, Vijana ndio msingi wa maendeleo katika jamii, hivyo wana jukumu la kuhakikisha wanashiriki vyema katika kudumisha usalama ndani ya maeneo ili shughuli za maendeleo zifanyike kwa amani.

Aidha, alisisitiza kuwa ili kuhakikisha lengo la kudumisha amani pamoja na kuzuia uhalifu linatimia, wanapaswa kuwa mstari wa mbele kujiunga kwenye vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na kuhamasisha wengine ili kuendelea kuwa na jamii yenye usalama muda wote.

Katika hatua nyingine Mkaguzi huyo alikemea matumizi ya Dawa za kulevya ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa kikwazo cha maendeleo kutokana na kuathiri uwezo wa Vijana wa kushiriki shughuli za maendeleo katika jamii.

Elimu hiyo ni muendelezo wa kuwafikia Vijana vijiweni, ili kuhamasisha uanzishwaji na ushiriki wao katika vikundi vya ulinzi shirikishi katika shehia.

TANESCO kateni Umeme kwa wanaodaiwa - Dkt. Biteko
Vijana wahimizwa kufanya kazi, kutokukaa vijiweni