Jeshi la Polisi Mkoani Tanga, limewaonya madereva wanaoendesha Magari kuachana na udereva wa kimazoea na badala yake wafuata Sheria za Usalama Barabarani.
Kauli hiyo, imetolewa na Mkaguzi wa Magari kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga Mkaguzi wa Polisi, Rajab Ngumbi wakati akizungumza na madereva hao katika Kituo cha Polisi Traffic Mabawa.
Amesema, Dereva yeyote atakayebainika kuzidisha abiria au kukutwa na nyaraka batili atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kwamba kila dereva anapaswa kufanya uhakiki wa leseni yake, kutembea na barua ya uhakiki, kutembea na leseni halisi za udereva na kuepuka mwendo kasi.
Aidha, Ngumbi amebainisha kuwa Dereva atakaye kamatwa kwa makosa yeyote ya uvunjifu wa Sheria za Usalama Barabarani, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria.