Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino amepandwa na “hasira” baada ya timu yake kupokea kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Newcastle katika mchezo wa Ligi Kuu ya England juzi Jumamosi (Novemba 25).

Wenyeji Chelsea walisawazisha kabla ya kipindi cha pili, lakini walijikuta wakilowa baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza, huku wakipata pigo baada ya nahodha wake, Reece James kutolewa nje.

Baada ya kucheza vizuri katika mchezo dhidi ya Tottenham Hotspur na Manchester City, Pochettino alihisi Chelsea walikuwa wepesi kila walipokuwa wakiwania mpira katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa St James’ Park.

“Kwa kweli hatukuonesha kama tulikuwa tunacheza kitu fulani muhimu. Hata kama Newcastle hawakuwa wakubwa, ulikuwa ni ushindi mwepesi kwao kwa ajili ya kujiandaa na Ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Ilitakiwa kuoneha kuwa tuko tayari kwa mchezo mgumu na wangeshindwa kutufunga.”

“Lakini kwa kweli ilikuwa rahisi sana kuruhusu magoli na hatukufanya vizuri katika kila eneo. Hilo ndilo limenifanya kukasirika na kukata tamaa. Tulizungumza kuhusu timu change na tunatakiwa kujifunza, aina hii ya mchezo imenifanya mimi kuwa na hasira sana…”

“Sawa, bado hatujakomaa kama timu, lakini hatuwezi kushindwa kama hivi tulivyonesha leo, tulikuwana nafasi ya kuonesha ubora uwetu.”

Gamondi: Hatutakubali kufungwa nyumbani
Wachezaji Simba SC wafunguliwa milango