Kocha Mkuu wa Young Africans Miguel Angel Gamondi amesema kuwa wanakwenda kukutana dhidi ya Mabingwa wa Soka Barani Afrika Al Ahly ya nchini Misri wakiwa na hasira za kutoka kufungwa na CR Belouizdad, hivyo hawatawaacha wapinzani wao hao.

Young Africans walipoteza mchezo wao wakwanza wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Mabingwa wa Soka wa Algeria CR Belouizdad kwa mabao 3-0.

Young Africans itajitupa tena kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam kukipiga dhidi ya Al Alhly mwishoni mwa juma hili.

Gamondi amesema kuwa wanakwenda kucheza dhidi ya Al Ahly malengo yao ni ushindi na siyo kitu kingine.

Gamondi amesema kuwa hawatakubali kupoteza mchezo kwa mara ya pili mfululizo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika na badala yake wanahitaji ushindi pekee.

Ameongeza kuwa ameona upungufu wa kikosi chake ambao ataufanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi kuhakikisha kikosi chake kinakuwa tayari kwa ajili ya ushindi.

“Mashabiki wetu wameumizwa na matokeo ya mchezo uliopita dhidi ya CR Belouizdad tuliocheza Algeria, pia mimi na wachezaji wangu yametuumiza.

“Licha ya kuumizwa na matokeo hayo, kikubwa tunachotakiwa ni kusahau matokeo hayo na badala yake kujipanga kwa ajili ya mchezo ujao.” Amesema Kocha huyo kutoka nchini Argentina

Abdelhak Benchikha kupitisha panga Simba SC
Wachezaji Chelsea wabebeshwa zigo