Kocha Mpya wa Simba SC amekiangalia kikosi cha timu hiyo katika mchezo dhidi ya Asec Mimosas na kugundua kuwa kuna safari kubwa anayo, ya kuhakikisha kuwa anarudisha hali ya kujiamini na kuifanya klabu hiyo kurudi kuwa tishio kama awali.

Benchikha alifanikiwa kuutazama mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Asec Mimosas ambapo katika mchezo huo alishuhudia timu yake ikitoka sare ya bao 1-1.

Taarifa za awali kutoka ndani ya Simba SC zinaeleza kuwa katika makubaliano ya kocha huyo mpya na uongozi wa timu hiyo ni pamoja na kufanya maboresho ya wachezaji kwa kuwaondoa wachezaji wengi wenye umri ulioenda, jambo ambalo kocha huyo amebaini kuwa ni tatizo ndani ya timu hiyo ambapo ameomba uongozi ufanye usajili wa maana katika madirisha mawili yajayo ili kuirudisha Simba katika ubora wake.

“Kocha tayari amekiangalia kikosi cha Simba SC na kubaini kuwa tatizo kubwa lingine ambalo linaisumbua timu hiyo ni pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wachezaji ambao umri wao umeenda.

“Wachezaji kama Saido Ntibazonkizá, Shomari kapombe, John Bocco na Clatous Chama ni baadhi ya wachezaji ambao wapo kwenye taa nyekundu kutokana na umri wao, kocha amesema kuwa wanachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa uongozi unafanya usajili wa maana katika madirisha mawili yajayo na wachezaji wenye umri mzuri ili kuendana na kasi yake,”kilisema chanzo hiko.

Hata hivyo uongozi wa Simba SC chini ya mwenyekiti, Salim Abdallah Try Again baada ya mchezo kumalizika kwa sare dhidi ya Asec Mimosas walifanya kikao cha dharula na wachezaji kwa masaaa mawili ambapo wamekubaliana baadhi ya mambo ili kuona timu inafanya vizuri.

Meneja wa Habari na Mawasilino Simba SC Ahmed Ally amesema kuwa “‘Simba SC kwa sasa bado tunajitafuta lakini muhimu ni kuhakikisha kuwa tunakwenda hatua inayofauata katika michuano ya kimataifa, tutapambana na wachezaji wametuahidi kuwa wataipigania timu.”

Aaron Ramsdale amfurahisha Kocha Arsenal
Gamondi: Hatutakubali kufungwa nyumbani