Klabu ya Al-Ettifaq ya Saudi Arabia inadaiwa kutaka kumsajili Mlinda Lango kutoka Hispania, David de Gea katika dirisha lijalo la usajili wa majira ya baridi licha ya kipa huyo kukataa ofa ya mshahara wa Pauni 500,000 kwa juma kujiunga na Al Nassr katika wiki chache zilizopita.

De Gea kwa sasa ni mchezaji huru tangu aachane na Manchester United katika dirisha lililopita. Alikataa ofa ya kutua Al Nassr na taarifa zikadai anataka kutua Inter Miami.

Ettifaq kupitia kocha wao Steven Gerrard haijakata tamaa na inataka kumzidishia dau kutoka lile ambalo Al Nassr walihitaji kumpa ili tu akubali kutua kwenye kikosi chao.

De Gea alikataa kutua Saudi Arabia baada ya kuhitajika hapo awali kwa sababu familia yake haipendezwi kuishi nchini humo na badala yake wanapendela zaidi mazingira ya Marekani ama kubakia nchini Hispania ambako ndio nyumbani kwao kabisa.

Staa huyo pia alihusishwa na kurudi Man Utd Januari 2024, Onana atakapokwenda kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika AFCON 2023 kujiuinga na kikosi cha Cameroon.

Wakwamishaji changamoto za Walimu kukiona
Vijana waongoza maambukizi mapya ya UKIMWI