Viongozi, Wachezaji na Benchi la Ufundi jipya linaoongozwa na Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha wamefikia makubaliano ya mchezaji yeyote atakayezingua, basi anawekwa pembeni.

Maamuzi hayo yametolewa baada ya kufanyika kikao kizito kilichowahusisha Wachezaji, Viongozi na Benchi la Ufundi, mwanzoni mwa juma hili.

Kwa mujibu wa Mmoja wa Viongozi kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la timu hiyo, kwa pamoja Wachezaji wamekubaliana na uongozi sasa hakuna aliyekuwepo juu ya timu kwa kuanzia wachezaji hadi viongozi.

Kiongozi huyo amesema kuwa wachezaji hao wameenda mbali zaidi, kwa kuwataka viongozi wasimuangalie usoni mchezaji yeyote atakayekwenda kinyume na utaratibu wa timu, badala yake kuwajibishwa mara moja.

Ameongeza kuwa wachezaji hao waliwataka viongozi kutomuingilia kocha huyo katika upangaji wa kikosi chake, badala yake aachwe aamue mchezaji wa kuanzishwa katika timu.

“Maamuzi mazuri yamefikiwa baada ya kikao kizito kufanyika katika Wachezaji, Viongozi na Benchi la Ufundi, mengi yamezungumzwa katika kuboresha mambo muhimu.

“Baadhi ya wachezaji wameenda nbali zaidi na kusema, hata akitokea mchezaji akienda kinyume cha utaratibu, basi viongozi wasiangalie ukubwa wa jina na baadala yake wamuwajibishe haraka.

“Pia kocha asiingiliwe majukumu yake kwa aina yoyote ile baada ya kupewa taarifa zote hali halisi ya maisha yetu na tabia zetu kama Watanzania,” amesema Kiongozi huyo.

Mtendaji Mkutu wa timu hiyo, Imani Kajula alizungumzia hilo kwa kusema kuwa: “Uongozi hautamuingilia kocha wetu mpya katika maamuzi yake ya kupanga kikosi pamoja na usajili.

“Hivyo tutaamuacha afanye kazi yake kwa uhuru, ili kuhakikisha tunarejea katika ubora wetu katika michezo ijayo ya ligi na michuano ya kimataifa.”

Gavi kurudi FC Barcelona 2024/25
Klabu za England zamuwania Jean-Clair Todibo