Mshambuliaji kutoka DR Congo na Klabu ya Azam FC, ldris Ilunga Mbombo atakuwa nje ya uwanja kwa takribani majuma matatu baada ya kusumbuliwa na jeraha la goti.
Akizungumza na jijini Dar es salaam daktari wa timu hiyo, Mbaruku Mlinga amesema nyota huyo alianza kusikia maumivu katika mchezo na Mashujaa uliopigwa Novemba Mosi mkoani Kigoma ingawa ilionekana sio siriasi kama ilivyo sasa.
“Baada ya hapo aliendelea vizuri na prograrmu za mazoezi na wachezaji wenzake ila alijitonesha tena sehemu ya goti lake wakati wa mchezo na Ihefu kule Mbeya hivyo ilimfanyia vipimo kugundua ni jeraha ambalo ni siriasi kidogo.” amesema.
Mlinga ameongeza baada ya vipimo vya awali imegundulika atakuwa nje kwa wiki tatu huku akiwa kwenye uangalizi mzuri wa madaktari.
Kwa upande wa Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Youssouph Dabo amesema ni bahati mbaya kwao na kwa nyota huyo kwani wao kama Benchi la Ufundi hufurahia kuona wakiwa na wachezaji wote hasa katika kipindi hiki ambacho cha Ligi wana michezo mingi muhimu.
“Kila kocha anapenda kuona akiwa na wachezaji wake bora kikosini kwa sababu inatoa wigo mpana wa machaguo kutokana na aina ya mpinzani tunayekutana naye, ni bahati mbaya kwake lakini ni nafasi kwa wengine kuonyesha ubora waliokuwa nao.