Mchambuzi wa Soka nchini England kupitia kituo cha Televisheni cha Sky Sports na mkongwe wa Klabu ya Liverpool, Jamie Carragher amesemna Arsenal ya kawaida sana tofauti ilivyokuwa msimu uliopita.

Garragher amedai anafatilia mechi zao zote na anaamini kuna uwezekano mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England zikakwama kutokana na kiwango chao msimu huu.

Hata hivyo, Arsenal imepanda nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Brentford wikiendi iliyopita ikiwazidi Manchester City kwa tofauti ya pointi moja tu.

Huo unakuwa ushindi wa tano kwa Arsenal baada ya mapumziko ya kimataifa huku Kai Havertz akiibuka shujaa kwani alifunga bao la ushindi dakika ya 89 akitokea benchi.

Mkongwe huyo akadai Arsenal bado inakabiliwa na changamoto katika safu ya ushambuliaji hivyo Kocha Mikel Arteta ana kazi ya kufanya kama amepania kubeba ubingwa, kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2003-2004.

“Bado tumebaki na nusu ya msimu, kama Arsenal itaendelea kucheza hivi na kiwango kidogo sidhani kama ina nafasi ya kubeba ubingwa msimu huu, mechi za ligi zina upinzani mkali, tuliona makosa ya kipa Aaron Ramsdale dhidi ya Brentford wikiendi iliyopita, angeigharimu timu na tuliona Arsenal ilivyopambana kupata ushindi kipindi cha pili.”

Carragher akasisitiza Arsenal imekosa muunganiko na nguvu ambayo iliwafanya kuwa hatari msimu uliopita licha ya kukosa ubingwa zikiwa zimebaki mechi tano msimu ligi kumalizika.

“Nadhani tunaiongelea Arsenal tofauti msimu huu, hata takwimu zao unaona msimu huu, lakini kila mtu ataona kwa macho yake, Arsenal sio kama ya msimu uliopita, haina nguvu, hata nafasi wanazotengeneza ni chache sana. Hata safu yao ya ushambuliaji yao imekuwa ya kawaida sana.”

Hiyo sio kauli ya kwanza kuhusu uwezo wa Arsenal katika kinyang’anyiro cha ubingwa, mkongwe wa Manchester United, Gary Neville aliwahi kutabiri kwamba kikosi Arsenal hakina uwezo wa kubeba ubingwa wa ligi msimu uliopita.

Tabora United yachimba mkwara Ligi Kuu Bara
Benchikha akataa mifumo ya Robertinho