Serikali ipo kwenye maandalizi ya awali ya ujenzi wa kampasi 14 mpya za vyuo vikuu kwenye mikoa ya pembezoni isiyokuwa na vyuo
vikuu. 

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Mkoani Iringa huku akiitaja mikoa hiyo kuwa ni Kigoma, Ruvuma, Singida, Mwanza, Kagera, Tanga, Njombe, Tabora, Manyara, Simiyu, Shinyanga, Lindi, Rukwa, na Katavi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu cha Iringa kwenye viwanja vya Chuo hicho mjini Iringa, Novemba 30, 2023.

Amesema, “hatua hiyo ni moja ya jitihada za makusudi za Serikali za kuharakisha ukuaji wa uchumi kwenye maeneo ya pembezoni, kuongeza nafasi za elimu ya ufundi, ujuzi na stadi za maisha katika maeneo hayo ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa fursa za elimu na ajira.”

Akielezea uboreshaji wa miundombinu ya vyuo vikuu, Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita inaendelea na ujenzi wa miundombinu muhimu ambayo ni vyumba vya mihadhara, maabara, nyumba za walimu na maktaba.

Baadhi ya wahitimu wa Mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu cha Iringa wakimsiliza Waziri Mkuu

“Kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Serikali inaendelea na ujenzi wa mabweni 34; vyumba vya mihadhara na madarasa 130; kumbi za mikutano ya kisayansi 23, maabara/karakana za kufundishia 108, miundombinu ya shambani na vituo atamizi 10,” alisema.

Aidha Amesema kukamilika kwa ujenzi huo kunatarajiwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma programu za kipaumbele (STEM) kutoka wanafunzi 40,000 kwa mwaka 2020 hadi kufikia 106,000 mwaka 2026.

Ally Kamwe: Al Ahly itatupandisha viwango Afrika
Lautaro Martinez kuzipotezea Chelsea, Man Utd