Gwiji wa Soka nchini England Paul Scholes amejibu shutuma za Bruno Fernandes baada ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya Galatasaray, kwa kumwambia nahodha huyo wa Manchester United anatakiwa kuwajibika kutokana na makosa aliyofanya.

Hiyo imekuja baada ya kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno kuwatolea maneno makali wachezaji wenzake katika mahojiano baada ya mechi, akidai kiwango cha timu bado hakitoshi.

“Najua katika mahojiano anazungumzia makosa, lakini alifanya makosa mawili makubwa katika mechi, alisababisha faulo mbili, timu pamoja naye wanapaswa kuwajibika kutokana na makosa, ni mechi ambayo walipaswa kushinda, ameshindwa kutoa pasi sahihi, safu ya beki ilikuwa nzuri, Onana alizingua na imefanya mechi kuwa ngumu sana.” amesema Scholes.

Ikumbukwe, Man United itakuwa na kibarua dhidi ya Newcastle kesho Jumamosi (Desemba 02) kwenye mechi ya Ligi Kuu England.

Gamondi atamba kuibomoa Al Ahly
Kocha Al Ahly aivimbia Young Africans