Ili kukabiliana na kasi ya kuenea kwa maambukizi wa VVU, Wizara ya Afya imezindua mpango wa kuoanisha VVU, magonjwa ya ngono na homa ya ini kwani kuna ushabihiano mkubwa wa njia za maambukizi za magonjwa hayo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu hii leo Desemba mosi, 2023 katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Morogoro, mjini Morogoro.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Amesema, hatua hiyo imekuja baada ya kubaini kuwa asilimia 4.4 ya Watanzania wana maambukizi ya magonjwa ya ini.

Kuhusu mpango wa wizara kufikisha huduma ya afya kwa ngazi ya jamii, Waziri Ummy amesema Wizara hiyo inatarajia kuajiri wahudumu wa afya ya jamii 137,000 ambao watafanya kazi kuanzia ngazi ya mitaa na vitongoji.

Ronaldo kupandishwa kizimbani Marekani
Ajali nyingine ya Basi la Esther Luxury