Kile unachokula asubuhi kinaweza kutengeneza au kuharibu afya yako, na ndiyo sababu mlo au kinywaji cha kwanza cha siku kinachukua sehemu muhimu katika mlo wa kila siku.
Kwa mujibu wa wataalamu wa Afya, kinywaji au chakula cha kwanza cha siku kinaweza kusaidia kuboresha afya kwa ujumla kwa kutoa virutubisho vya kutosha, baada ya kulala kwa zaidi ya saa nane au kinaweza kusababisha usumbufu na magonjwa ya usagaji chakula.
Hapa kuna baadhi ya vyakula vya kawaida ambavyo lazima uepuke kutumia iwapo tumbo lako halijapata kitu (chakula) chochote.
- KAHAWA
Kunywa Kahawa huku tumbo lako likiwa halijapata kitu ni ibada ya kila siku kwa watu wengi, lakini itastaajabishwa kujua kwamba kunywa kahawa nyeusi au kahawa na maziwa kunaweza kuchochea uzalishaji wa asidi ndani ya tumbo, ambayo inaweza kusababisha matatizo ya usagaji wa chakula na usumbufu wa gesi.
- VYAKULA VILIVYOKAANGWA
Kula vyakula vilivyokaangwa au vitafunio asubuhi kunaweza kukufanya uhisi tumbo kujaa siku nzima, hii ni kwa sababu ya tabia ya juu ya aina ya mbalimbali za mafuta yaliyotumika, ambayo yanaweza kuwa mazito tumboni. Kutumia vyakula hivyo huku tumbo lako likiwa halijapata kitu chochote kunaweza kusababisha kutokula chakula na hata kukufanya uhisi uchovu.
- MACHUNGWA
Kuanza siku yako kwa kula Matunda ya machungwa au juisi yake kunaweza kusababisha kuongezeka kwa asidi na kunaweza kusababisha usumbufu na kiungulia. Katika baadhi ya matukio, vyakula hivi vinaweza kuingiliana na asidi ya utumbo ndani ya tumbo na uwepo wa asidi nyingi na kukusababishia vidonda.
- NDIZI
Ingawa ndizi kwa ujumla huchukuliwa kuwa tunda lenye afya, watu wengine wanaweza kupata usumbufu wanapokula tunda hili ikiwa hawakula kitu kingine chochote kwani Ndizi hupelekea kiwango cha juu cha magnesiamu na potasiamu hivyo kukupa gesi.
- NYANYA
Nyanya ni tunda lenye tindikali kwa asili hili halipingiki na kuzitumia kwa namna ya saladi, juisi au chombeza inaweza kusababisha wingi wa asidi baada ya kula / kunywa kwenye tumbo lililo tupu.
Kiuhalisia kula kiasi kikubwa cha viungo vya aina tofauti katika mlo wa asubuhi, inaweza kusababisha utando wa tumbo kudhurika na pia inaweza kusababisha kushindwa kwa usagaji wa chakula au mtu husika kupata kiungulia iwapo itatumiwa na mtu yeyote ambaye tumbo lake halijapata chochote tangu kuamka kwake.
Cha kuzingatia ni kuepuka ulaji wa vyakula tajwa na vinginevyo ambavyo vinafafanana ili kuepuka kupata madhara mbalimbali yanayoweza kupelekea muhusika kudhuruika, pia inashauriwa ukipatwa na hali hiyo waone wataalamu wa masuala ya Afya ya lishe wao wamebobea na watakupa njia sahihi za kuchukua ikiwemo tiba.