Johansen Buberwa, Bukoba – Kagera.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima amesma idadi yavifo vya watu waliopata ajali eneo la Kyetema lililopo Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera, vimeongezeka kotoka waru wanne hadi kufikia watu sita.

DC Sima ameyasema hayo hii leo Desemba 5, 2023 wakati akifanya mahojiano na Dar24 Media hii leo na kuongeza kuwa na idadi ya majeruhi wa ajali hiyo bado inasalia ileile ya Watu 19 ambao wanaendelea na matibabu.

Vifo hivyo, vimetokana na jali ya gari aina ya Totota Hiace na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi wa Polisi, Zablon Chatanda.

Hili linatokea huku Taifa likiwa na majonzi ya vifo vya takribani watu zaidi ya 64 vilivyotokana na mafiriko yaliyosababisha maporomoko huko Katesh Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara.

Askari waliofariki kwa ajali Njombe waagwa
Uhakiki Malori ya vimiminika hurahisisha ukadiriaji wa bei - Mavunde