Mahakama Kuu ya Mombasa, imekubali ombi la Polisi la kuomba siku saba zaidi za uchunguzi, dhidi ya mwanamke aliyemtupa mwanawe Baharini kwenye kivuko cha Likoni Feri mjini Mombasa.

Mwanamke huyo, Beatrice Wakio ambaye ni Mlemavu wa Kuzungumza, alimtupa mwanaye Baharini siku ya Jumapili Desemba 3, 2023 kwenye kivuko cha Likoni wakati usafiri huo ukitoa nanga.

Matukio ya utupaji watoto wachanga yamekuwa yakishika kasi, ambapo Oktoba 13, 2023 katika Manispaa na Mkoa wa Morogoro kuliibua taharuki kwa wakazi wa eneo hilo, baada ya kukuta watoto mapacha wanaokadiriwa kuwa na umri wa siku moja wakiwa wametupwa porini, huku miili yao ikiwa kwenye mfuko.

Mkuu wa Idara ya Watoto Hospitali ya Rufaa mkoa wa Katavi Dkt. Maria Matei mapema mwaka huu pia alithibitisha kumpokea mtoto mchanga mwenye umri wa siku mbili, aliyenusurika kufa baada ya kutupwa chooni na mama yake mzazi, mara baada ya kuzaliwa katika kijiji cha Uruwila, kilichopo Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.

Picha: Mafuriko Kilosa yalivyosababisha kifo
Tahadhari yatolewa matukio mwisho wa mwaka