Manchester United wanapanga kumsajili Mlinda Lango wa AC Milan, Mike Maignan, kwa mujibu wa ripoti.

Mashetani wekundu tayari wanatafuta Mlinda Lango mpya licha ya kumsajili Andre Onana majira ya joto mwaka huu.

Onana alijunga na Mashetani Wekundu akitokea Inter Milan Pauni Milioni 47 akichukua nafasi ya David de Gea ambaye mkataba wake ulimalizika.

Hata hivyo, tangu wakati huo amekuwa akikosolewa baada ya makosa kadhaa makubwa ikiwa ni pamoja na aliyofanya dhidi ya Galatasaray juma lililopita.

Masaibu yake hayo yamemfanya hata kufikiria kujiondoa timu ya Taifa ya Cameroon ambayo itashiriki Kombe la Mataifa ya Afrika Januari mwakani akihofia kama ataondoka basi nafasi yake inaweza kuchukuliwa na kipa mwingine.

Lakini hata hivyo hivi karibuni anaweza kukutana na kitu kizito kwani United iko siriaz inataka kumsajili kipa wa AC Milan, Maignan.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka majuu, United wameonyesha dhahiri kuhitaji huduma ya kipa huyo Mfaransa ambaye pia anahusishwa na Chelsea, PSG na Bayern Munich.

Maignan, ambaye thamani yake inaweza kufikia Pauni Milioni 60, anataka kubaki Milan lakini bado hajakubali mkataba mpya.

Marekani waunga mkono mradi kutokomeza ukeketaji
Dkt. Tulia awajulia hali majeruhi wa maafa Hanang'