Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, amewatembela na kuwajulia hali majeruhi wa maafa ya mafuriko ya matope na mawe yaliyotokea Wilaya ya Hanang’ ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.

Dkt. Tulia amewatembelea majeruhi hao hii leo Desemba 6, 2023 na kuipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa uharaka na kazi nzuri ya kuhudumia waathiriwa hao ma mafuriko yaliyotokea Jumapili ya Desemba 3, 2023.

Aidha, Dkt. Tulia pia ameipongeza timu ya Madakatri waliotoka Mikoa ya jirani kufika mapema katika Hospitali ya hiyo ili kuongeza nguvu kwa ajili ya kuhudumia majeruhi.

Jana, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pia alitembelea kambi ya muda ya waathirika wa maafa ya mafuriko yaliyosababisha kuharibika kwa nyumba na miundombinu kutokana na maporomoko ya tope na mawe kutoka Mlima Hanang’ huko Katesh, Mkoani Manyara.

Man Utd yamsaka mbadala wa Onana
Kocha Coastal Union afurahia kazi