Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wamekamilisha usajili wa winga wa Granada, Bryan Zaragoza, ambaye atakuwa mbadala wa Harry Kane.

Mabingwa hao wa Bundesliga wamethibitisha kumsajili winga huyo kwa Pauni 13 milioni kwa mujibu wa Sky Sport kutoka Ujerumani.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amesaini mkataba wa miaka mitano na ataanza kuonekana uwanjani msimu wa 2024-25.

Mkurugenzi wa Michezo wa Bayern, Christoph Freund alisema katika taarifa rasmi:  “Bryan Zaragozani winga mwenye nguvu, mwenye kasi sana na mwepesi sana ambaye anaweza kutumika pande zote mbili. Yeye hatabiriki, Tayari ameshacheza kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya wakubwa ya Hispania mwaka huu na ana uwezo mkubwa.

Bryan ni mmoja wa wachezaji hatari Hispania, amekuwa kwenye rada yetu kwa muda mrefu. Ataleta changamoto kikosini. Tunamtakia kila la heri kwa muda wote atakaokuwa Granada.”

Freund alishinikiza uhamisho ukamilike kwa muda mrefu kwani alikuwa na ndoto ya kuichezea Bayern na atachuana vikali na Kane msimu ujao.

Kuwasili kwa Zaragoza bila shaka kutaimarisha kikosi cha Thomas Tuchel lakini kwa sasa hata hivyo ataendelea kubaki Granada kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.

Afrika iweke mazingira bora ya biashara - Othman
Mafunzo BBT: Nidhamu, Utii vyawabeba Vijana JKT