Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewapongeza Vijana waliokuwa kwenye mafunzo ya mradi wa Jenga kesho iliyobora – BBT, kwa kuonyesha uvumilivu na nidhamu kwa kipindi chote walipokuwa kwenye mafunzo katika kikosi 834 KJ Makutupora, Jijini Dodoma.

Bashe ameyasema hayo hii leo Desemba 8, 2023 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo ya kundi maalum BBT OP na miaka 60 ya JKT, na kuopngeza kuwa juhudu kubwa walizozizifanya mafunzoni ni ishara tosha ya lengo la Serikali kutimia katika kuinua uchumi wa Taifa.

Amesema,“kupitia juhudu ambazo mmezionyesha katika mafunzo mtakuwa mmejifunza kupenda kazi, kujituma, stadi za maisha pamoja na kuinua uchumi wenu binafsi na uchumi wa Taifa letu na kuanzia program zijazo zote za BBT zitaingia JKT, ili Vijana waweze kuwa imara kwa viwango tunavyovitegemea.”

Waziri Bashe ameongeza kuwa, Vijana wanaoendelea na BBT ni 688, Waliopo JKT 533 na wenye ruhusa 155 na kwamba wanatafuta Vijana ambao watawekeza kwa Jamii pamoja na Nchi, wenye uvumilivu na nidhamu ili kunyanyua zaidi uchumi huku akiwashukuru kwakuwa makamanda wavumilivu.

Kwa upande wake Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajab Mabele amewaasa Vijana hao kuzingatia kiapo chao popote pale watakapokuwepo na katika na kwamba wakawe waipende kazi na kuwa hodari matika mazingira yoyote watakayokutana nayo.

Bryan Zaragoza anasubiri kazi Bayern Munich
Konkoni aongeza mzuka Young Africans