Afara Suleiman, Hanang’ – Manyara.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema idadi ya vifo vilivyotokana na Mvua iliyosababisha maporomoko Wilayani Hanang, imeongezeka na kufikia watu 80.
Matinyi ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kudai kuwa tayari Wataalamu wa Serikali wamekamilisha uchunguzi wa Kisayansi wa chanzo cha janga hilo na kuweka mipaka kwa kufuata mkondo wa mto Jorodom wa mlima Hanang.
“Eneo hilo ni la kati ya mita 60 na300 kutegemeana na ardhi ilivyokaa, ambapo Wananchi hawataruhusiwa kujenga makazi wala kufanya shughuli za kiuchumi katika eneo hilo kutokana na ukweli kwamba ni eneo hatarishi,” alisema Matinyi.
Hata hivyo, dadi hiyo ni ya mpaka saa sita mchana wa Desemba 8, 2023 na miongoni mwa marehemu hao, watu wazima ni 48 (Wanaume19), Watoto 32 (Wakiume 15), ambapo tayari miili 79 imeambuliwa.
Aidha, Matinyi amesema majeruhi 133 walipokelewa katika Hospitali mbalimbali za Mkoani Manyara, huku wengine 440 wakihudumiwa katika kambi za waathirika.