Mtu mmoja, Muhamed Abdalah Athuman (43), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Njombe kwa tuhuma za kufanya upasuaji wa Mabusha na Tezi dume, bila kuwa na Vyeti.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mahamoud Hassan Banga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa mtuhumiwa ni Mkazi wa Kijiji cha Mapogolo Wilayani Ludewa, ambaye anajihusisha na utaalamu wa tiba za asili.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mahamoud Hassan Banga.

“Anasema ni Mtaalamu wa tiba lakini hana vyeti, tumemkamata akiwa na vifaa tiba mbalimbali boksi zaidi ya 23 na amekuwa akiwatibu Watu akifanya upasuaji wa kuondoa mabusha na upasuaji wa tezi dume bila kuwa na vyeti,” alisema Kamanda Banga.

Mtuhumiwa huyo, pia alikamatwa akiwa na boksi zaidi ya 23 za vifaa tiba ambapo pia Kamanda Banga amesema wanamshikilia Dereva Bodaboda, Ibarahim Mgimba (25), kwa tuhumiwa za kuhusika na usafirishaji wa bidhaa hizo ili kuzificha wakati Polisi wakimtafuta Mtuhumiwa huyo.

Ushirikina, ugomvi kikwazo Mashujaa FC
Singida FG yakutana na rungu lingine FIFA