Utamaduni wa Makabila yetu wakati mwingine huwa unatafakarisha na waweza kaa na ukatafakari kwa kina ukakosa majibu sahihi kwani utabakia kushangaa na kuhoji bila usaidizi wa ufumbuzi.

Kuna Kabila la Dani linapatikana Nchini Indonesia, huko Wanawake hukata ncha za kidole kimoja kila Mwanafamilia anapokufa, wakiamini hiyo ni njia sahihi ya kuomboleza na kuonesha huzuni yao na kibaya zaidi eti wanairidhisha mizimu ya mababu zao.

Wanachofanya ni kutia ganzi kidole chao kwa dakika 30 kwa kufunga kamba kwa nguvu inayozunguka kidole na kisha kukikata. Baada ya hapo, watalitia jeraha kwa moto na kisha kuendelea na ratiba zao nyingine.

Lakini utamaduni ni nini? Wikipedia inatueleza kuwa ni jinsi binadamu anavyokabili maisha katika mazingira yake ikijumuisha ujuzi, imani, sanaa, maadili, sheria, desturi n.k. ambavyo mtu anajipatia kama mwanajamii.

Na hii ni sifa maalumu ya binadamu inayomtofautisha na Wanyama, yaani ni suala la msingi katika uwasilishaji wa yale yoye yanayofanywa katika jamii fulani, ikiwemo na lugha inayounganisha watu wanaohusika nao, fasihi, mafungamano, ndoa, michezo, ibada, sayansi na teknolojia.

Hili huendana pia na Mila, ambazo pia nazo ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao, ikitambulisha pia maadili ya jamii husika.

Mageuzi yamesaidia ufikiwaji wa huduma - Dkt. Mwinyi
Hiki ndio chanzo cha kifo cha mwimbaji Zahara